Categories
Kimataifa

Uingereza: Nani kuwa Waziri Mkuu ajaye

Kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Lizz Truss, macho yameelekezwa kwa chama cha wahafidhina (Conservatives) ambako atapatikana mrithi wa nafasi hiyo.

Hadi sasa majina matatu ndio yanatajwa zaidi. Rishi Sunak, aliyebwagwa na Truss kwenye kinyang’anyiro kilichopita kuwania uongozi wa chama hicho kufuatia kujiuzulu kwa Boris Johnson, anatajwa kuwa anaongoza kwenye idadi ya wanaomuunga mkono ndani ya chama hicho.

Hata hivyo, upinzani mkali kwa Rishi, Muingereza mwenye asili ya Bara la Asia, unatoka kwa Boris, ambaye wafuasi wake wanataka arudi tena madarakani licha ya “madudu” lukuki yaliyougubika utawala wake.

Mwanasiasa mwingine ni mwanamama Penny Mordaunt ambaye hata hivyo baadhi ya misimamo yake isiyo ya kihafidhina inampunguzia sapoti.

Vyovyote itakavyokuwa, kiongozi ajaye wa chama hicho, ambaye ndiye atakuwa Waziri Mkuu, atafahakika Ijumaa.

Categories
Kimataifa

Saudi Arabia: Patashika baada ya fataki kudhaniwa risasi wakati wa ziara ya Waziri wa Ulinzi kwenye ubalozi wa China (VIDEO)